Monday, 4 July 2016

Hela

180. Shetani akikupa hela chukua. Hiyo hela ameiiba kutoka kwa Baba. Ukishaichukua, toa zaka.

http://www.facebook.com/koloniasantita 

3 comments:

  1. Katika dunia ya leo ambapo mamilioni ya watu hutegemea utandawazi kupata pesa, kuwa na imani kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua au mtu mwenye nia mbaya na wewe ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu, karibu kila mtu unayekutana naye ni Shetani. Shetani ni mtu yoyote mwenye nia mbaya na wewe. Hivyo, kama uliwahi kuambiwa kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ni kitu kibaya futa imani hiyo. Utaachaje kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua wakati kila siku unamwomba Mungu akusaidie, na Mungu hutenda kazi zake pale tunapojisahau? La sivyo hutapata pesa unayotamani kupata katika maisha yako, na kamwe hutawaamini watu. Zaka huondoa laana ya mapato. Toa zaka kununua pepo uliyopewa na Mungu.

    Mungu hataki tuwe maskini, kwani fedha na dhahabu ni mali yake. Anachotaka kutoka kwetu, zaka.

    ReplyDelete
  2. Pesa itolewe kwa masharti au bila masharti chukua, kwani huyo aliyeitoa si yake. Benki, kwa mfano, ikitaka kukupa mkopo itakuwa na masharti yake; chukua, iwapo utakubaliana na masharti hayo. Jambazi akikupa pesa ili ukafanyie ujambazi chukua pia. Lakini hiyo usiipeleke kanisani, ipeleke serikalini. Serikali itajua jinsi ya kupambana na huyo aliyekupa hiyo pesa, na hiyo pesa itaendelea kuimarisha ulinzi na usalama nchini. Pesa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama nchini ni sawa na zaka, au sadaka, na wewe utabarikiwa kwa kupata nyingine.

    ReplyDelete
  3. Kama huna uwezo wa kutoa zaka usipokee pesa kutoka kwa watu usiowajua. Shetani ana mitego mingi.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...