181. Damu, mto wa maisha unaotiririsha maji yake mwilini kwa kusukumwa 
na pampu za moyo na kuchujwa na fizi za mapafu, inaundwa na seli na maji
 yaitwayo utegili au maji ya damu, ambayo kazi yake ni kusafirisha 
oksijeni na virutubisho katika kila sehemu ya mwili, ndani yake kuna 
roho. Mungu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Adamu na Hawa katika 
Bustani ya Edeni. Ibrahimu alitoa kafara ya damu kwa ajili ya Israeli 
ijapokuwa mapenzi ya Mungu kwa Israeli yalikwisha baada ya kusulubiwa 
kwa Yesu Kristo. Wana wa Israeli walitoa kafara za damu kwa ajili ya 
wokovu wa watoto wao wa kwanza na watoto wa kwanza wa wanyama wao nchini
 Misri. Mungu alitoa kafara ya damu ya Yesu Kristo nchini Israeli kwa 
ajili ya wanadamu wote duniani. Damu ya mwanakondoo ina nguvu kuliko 
maombi, imetiwa wakfu na Mwenyezi Mungu na ina uhusiano mkubwa na 
ulimwengu wa roho. Ukifunikwa na damu ya mwanakondoo Shetani hatakuona. 
Shetani asipokuona, utafanikiwa.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Siku ya kwanza dhambi ya kwanza ilipotendwa Mungu alitoa kafara ya kwanza ya mnyama kwa ajili ya wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa. Adamu na Hawa walikuwa uchi, baada ya kutenda dhambi, Mungu akawalaani lakini akawapa uwezo wa muda mfupi wa kutubu dhambi zao ili awasamehe! Kutokana na ngozi za wanyama hao walipata mavazi na kutokana na damu ya wanyama hao walipata fursa ya kuishi na kutubu dhambi zote walizozitenda. Bila hivyo wasingepata muda wa kusamehewa.
ReplyDeleteKama damu haina maana kwa nini Mungu anaipenda? Kama damu haina maana kwa nini Shetani anaipenda? Mungu ni roho, Shetani ni roho, lakini damu ni kitu kinachoonekana kwa macho. Kwa nini damu ni kitu cha muhimu kiasi hicho kwa Mungu na kwa Shetani pia? Damu ni pato la ziada la ufunuo wa kiroho. Yaani, damu ni sehemu ya ulimwengu wa roho. Mungu ndiye aliyetengeneza damu kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe, hata Shetani hajui kwa asilimia mia umuhimu wa damu katika ulimwengu unaoonekana na katika ulimwengu usioonekana. Damu ina uwezo wa kuzuia mapepo kutoka kuzimu yasiharibu mipango ya maisha ya watu na ina uwezo wa kuondoa dhambi. Kafara ya damu inapotolewa inaimarisha uhusiano kati ya mtu na ulimwengu wa roho. Roho unayoitolea kafara inasikiliza shida zako papo hapo na kila unachoomba aghlabu kinatekelezwa. Ukitoa kafara kwa ajili ya Shetani, Shetani atasikiliza shida zako. Ukitoa kafara kwa ajili ya Mungu, Mungu atasikiliza shida zako. Tatizo kubwa la mwanadamu ni dhambi! Jibu la tatizo hilo ni damu ya Yesu Kristo. Imani ya mwanakondoo ni imani ya kweli! Imani ya mwanambuzi ni imani ya mashaka.