Monday, 13 June 2016

Asiyefundishwa

177. Asiyefundishwa na wazazi wake atafundishwa na dunia kwa kudharaulika.

http://www.facebook.com/koloniasantita

2 comments:

  1. Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu kingine chochote kile kwa sababu wana uwezo wa kuona tusipoweza kuona. Yaani, wanajua kilichokuwepo kabla ya sisi kuzaliwa na wanajua kilichokuwepo baada ya sisi kuzaliwa. Maisha tuliyopitia, wazazi wetu walishapitia. Tulipokuwa, wazazi wetu walishakuwepo; na tulichofanya, wazazi wetu walishafanya. Hivyo, hatuna budi kuwaheshimu wazazi wetu. Lakini, wazazi wetu wanapaswa kujiheshimu kutufundisha adabu na maadili mema.

    Mfundishe mtoto wako maadili mema kwa miaka kumi na tatu, katika umri wa miaka kumi na tatu fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali na watoto katika umri huo wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na hakika na hata zile zenye hakika zisizokuwa tata, kabla hujamkabidhi kwa dunia. Ukimkabidhi mtoto wako kwa dunia kabla ya umri wa miaka kumi na tatu, kama vile kumpeleka katika shule ya bweni au kumpeleka akalelewe na watu wengine ambao si wazazi wake, yale ambayo hukumfundisha atafundishwa na ulimwengu. Mpeleke mtoto wako katika shule ya bweni au kuishi na watu wengine akiwa amefundishwa maadili mema. Kinyume cha hapo atafundishwa na shule au watu wengine kwa kudharauliwa, kuchukiwa na kuadabishwa.

    Mwanampotevu dunia ilimfundisha ndiyo maana akarudi kwa baba yake akiwa amenyooka, hakuwa na maadili mema. Yusufu dunia ilimfundisha ndiyo maana akawa waziri mkuu wa Misri, na ndiyo maana akaokoa familia yake kutokana na njaa, alikuwa na maadili mema. Heri kudharaulika kwa kutenda mema kuliko kudharaulika kwa kutenda maovu. Ukidharaulika kwa kutenda maovu hutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukidharaulika kwa kutenda mema Mungu atakuinua.

    Wafundishe watoto wako uaminifu, adabu na jinsi ya kuishi vizuri na watu, ili waaminike, waheshimike na waishi vizuri na watu.

    ReplyDelete
  2. Kama baba yako hakukufundisha kwamba kuiba ni kitu kibaya, dunia itakufundisha kwa kukuchukia.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...