178. Siku moja, jambo baya litatokea. Labda babu yako au mnyama wako 
kipenzi atafariki au shangazi yako atagundulika na kansa. Labda 
utafukuzwa kazi au utaachika kwa mumeo au mkeo mliyependana sana. Labda 
rafiki yako kipenzi atapata ajali mbaya ya gari na utatakiwa kupeleka 
taarifa kwa ndugu na marafiki zake. Kutoa taarifa ya jambo baya kwa mtu 
ni kazi ngumu sawa na kupokea taarifa ya jambo baya kutoka kwa mtu. Kama
 umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya jambo lolote baya kwa mtu 
fanya hivyo kwa makini. Toa taarifa ya msiba au ya jambo lolote baya kwa
 hekima na busara kama Ibrahimu alivyofanya kwa Sara kuhusiana na kafara
 ya Isaka, si kama Mbenyamini alivyofanya kwa Eli kuhusiana na kutwaliwa
 kwa sanduku la agano na kuuwawa kwa watoto wake wawili. Jidhibiti 
kwanza wewe mwenyewe kama umeteuliwa kupeleka taarifa ya kifo au ya 
jambo lolote baya. Angalia kama wewe ni mtu sahihi wa kupeleka taarifa 
hiyo. Pangilia mawazo ya kile unachotaka kwenda kukisema au unachotaka 
kwenda kukiandika. Mwangalie machoni, si usoni, yule unayempelekea 
taarifa kisha mwambie kwa sauti ya upole nini kimetokea.
http://www.facebook.com/koloniasantita  
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Hakimu na Kuhani Mkuu wa Shilo Eli alipata matatizo makubwa wakati wa mgogoro wa Waisraeli na Wafilisti, kati ya mwaka 2870 na 2871 Kabla ya Kristo. Mara tu baada ya kupewa taarifa ya kifo cha watoto wake wawili, Hofni na Finehasi, na kutwaliwa kwa Sanduku la Agano la Bwana wa Majeshi lililohifadhi Amri Kumi za Mungu, Eli alianguka kutoka katika kiti chake na kufariki papo hapo akiwa na umri wa miaka 98. Aidha, mkwe wa Eli, mke wa Finehasi, alijifungua ghafla na kufariki alipopata taarifa ya kifo cha mkwewe na taarifa ya kuuwawa kwa mumewe na ya kutekwa nyara kwa Sanduku la Agano. Mwanajeshi kutoka Benyamini falaula angetumia hekima na busara kutoa taarifa ya kifo na ya kutwaliwa kwa Sanduku la Agano huenda Eli asingefariki, na huenda mkwewe asingejifungua mtoto njiti na huenda asingekufa siku hiyo. Kwani Sanduku la Agano lilirejeshwa nchini Israeli, na Wafilisti wenyewe, baada ya miezi saba tangu litwaliwe, na kifo cha watoto wa Eli yalikuwa mapenzi ya Mungu. Hivyo Eli asingeweza kuzuia kifo cha watoto wake, na Wafilisti wasingeweza kukaa na Sanduku la Agano.
ReplyDeleteLakini katika kafara ya Isaka ambapo Isaka aliamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake kama Yesu alivyoamua kujitoa kafara mwenyewe kumfurahisha Mungu na baba yake wa mbinguni, Sara angekufa kama Ibrahimu hangetumia hekima alipomwambia anakwenda kumtolea Bwana kafara ya mwanakondoo wakati akijua anakwenda kumtoa Isaka mtoto wa pekee wa Sara. Hekima inatoka moyoni, busara inatoka mdomoni. Kwa vile suala la kutoa taarifa mbaya kwa mtu ni gumu kwa yule anayetoa na kwa yule anayepokea, hekima na busara havina budi kutumika.