174. Msamaha si jambo rahisi. Tunapoumizwa, au watu wetu wa karibu
wanapoumizwa, tendo la kusamehe linaweza kuwa gumu kuliko matendo yote.
Lakini, tambua kwamba msamaha ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji
ujasiri mkubwa kuuanza hadi kuukamilisha, ongea na watu wanaoelewa maana
ya msamaha ili wakuongoze katika mchakato huo. Vilevile, tambua kwamba
hata wewe umewahi kufanya makosa na unahitaji msamaha, tambua kwamba
suluhisho kamili linahitaji matendo kutoka kwa aliyekosea na kwa
aliyekosewa. Wengine hupendwa kwa sababu wanastahili, lakini wengine
wanastahili kwa sababu hupendwa. Mungu anatupenda kwa jinsi tulivyo hata
kama tunajiona hatustahili. Hivyo, jithamini.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
120. Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu. http://www.enockmaregesi.wordpress.com
-
157. Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia. http://www.facebook...
Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.
ReplyDelete“Kama huwezi kumpenda mtu usimchukie.” – Enock Maregesi
ReplyDeleteWataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.
ReplyDeleteMsamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha.
ReplyDelete