Monday, 29 February 2016

Mungu

162. Katika dunia hii tunatakiwa kumwabudu Mungu peke yake. Si mtu au kitu kingine, chochote kile.

http://www.facebook.com/koloniasantita

1 comment:

  1. Lengo la kuabudu ni kumtukuza, kumheshimu, kumsifia, kumfurahia, na kumpendeza Mungu. Ibada yetu lazima ionyeshe mapenzi ya kweli na uaminifu mkubwa kwa Mungu kwa ajili ya wema na rehema ambavyo ametupa kupitia Mwanaye wa Pekee aliyekufa msalabani, ili kutuokoa kutoka ubinafsini.

    Watu wa zamani katika Agano la Kale walikuwa wakiabudu miungu iliyotengenezwa kwa mawe na vinyago. Miungu hiyo haikuwa na chochote ndani mbali na kutengenezwa kwa akili na fikira za kibinadamu. Hii ilikuwa ni kinyume cha ukweli wa Kibiblia kwamba Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake, lakini si mtu aliyejaa dhambi kumtengeneza Mungu kwa mfano wake. Kuabudu miungu mingine ni dhambi kubwa. Tii Amri Kumi za Mungu; hasa ya kwanza, ya pili na ya tatu.

    Musa alipokuwa mlimani kupokea Amri Kumi za Mungu kwa ajili ya Wana wa Israeli alikawia sana kurudi, kiasi cha watu kukata tamaa na kujiona wapweke wakiwa njiani kuelekea katika Nchi ya Ahadi. Kutokana na woga usio na kifani na kukata huko kwa tamaa waliamua kutosubiri tena kusikia neno kutoka kwa Mungu, au kuiona sura halisi ya Mungu kama Musa alivyokuwa amewaahidi, hivyo wakamlazimisha Haruni awatengenezee mungu kutokana na taswira ambayo tayari walishakuwa nayo vichwani mwao kuhusu mungu waliyemtaka; yaani ndama wa dhahabu, au mungu mpya ambaye angewapa chochote walichotaka muda wowote waliotaka.

    Mawazo ya kukata tamaa yanaweza kusababisha tukamtengeneza au kumbuni tena Mungu kwa mfano wetu sisi wenyewe, mfano ambao kwa kawaida ni tofauti kabisa na mfano unaozungumzwa ndani ya Biblia. Hivyo tunaishia kutumikia mfano badala ya kumtumikia Mungu wa kweli.

    Usimwabudu mungu mwingine isipokuwa Mungu. Usimwabudu mtu, mnyama, sanamu, samaki, au usiziabudu fikira zako kichwani. Usiitumikie kazi, mali, mila, anasa, siasa, wala usiyatumikie mamlaka au usiutumikie umaarufu au ufahari, kuliko Mungu. Ukiithamini kazi, mali, mila, anasa, siasa au ukiyathamini mamlaka, au ukiuthamini umaarufu au ufahari zaidi kuliko Mungu, au ukiyapa majukumu yako muda mwingi zaidi kuliko Mungu umeabudu miungu; wakati ulipaswa kumwabudu Mungu peke yake. Usiwe na vipaumbele vingine vyovyote vile katika maisha yako zaidi ya Mungu, kwani Mungu ni Mungu mwenye wivu.

    Mungu anataka tumwabudu Yeye na tuwe wavumilivu. Tusipomwabudu Yeye na kuwa wavumilivu hatatusaidia.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...