Thursday, 4 June 2015

G5

Bunduki yenye shabaha ya hakika na nzuri huenda kuliko zote duniani, G5 [G5 Gas Blowback Airsoft Rifle kutoka Taiwani]; iliyotumiwa na John Murphy katika 'hacienda' ya Panthera Tigrisi ya Coyoacán, Mexico City, Murphy akiwa katika harakati za kumwokoa Yehuda na Mogens, Radia Hosni akiwa hajulikani alipo, huku Debbie Patrocinio akisubiri katika gari kwa wasiwasi mkubwa.

http://www.enockmaregesi.wordpress.com

1 comment:

  1. Bunduki ya Kitaiwani yenye uwezo wa kubeba risasi arobaini katika chemba yake inayotumia gesi kufyatua risasi, G5, ambayo pia hutengenezwa na kiwanda cha GHK cha jijini Oklahoma nchini Marekani, ilitumika katika matukio mawili ya muhimu katika kitabu cha 'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi'. GHK-G5 ilitumika katika jumba la kifahari ('hacienda') la Panthera Tigrisi la Coyoacán, Mexico City; na katika Msitu wa Benson Bennett huko Salina Cruz, Oaxaca, nchini Meksiko. Katika jumba la kifahari la Panthera Tigrisi Murphy aliitumia kumwokoa Kanali Yehuda na Sajini Mogens; wakati katika Msitu wa Benson Bennett Radia aliitumia katika Operesheni ya Kifo au Ushindi Kamili ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.

    "Murphy akiwa bado amebana ukutani, ghafla yule mlinzi aliyekuwa akienda upande wake kwa hatua za haraka alisimama; akageuka na kurudi upande alikokuwa akitokea. Palepale Murphy alinyata na kutaka amshike lakini akashindwa na kujificha nyuma ya jiwe. Yule mlinzi alipofika katika kona aligeuka na kurudi tena upande wa Murphy ambako hakuona mtu. Alipofika katika jiwe lililomficha Murphy, yule mlinzi alipitiliza kidogo na kuwa sawa na Murphy lakini bila yeye kumwona kamanda. Nafasi hiyo ilikuwa nzuri na Murphy alihitaji kufanya haraka. Mithili ya chui Murphy alisafiri hewani. Kabla mlinzi hajajua nini kilikuwa kinaendelea, aliguna kareti mbili za utosi wake wa kichwa zilipomporomoka Murphy na akashindwa kupiga kelele. Shingo yake ilivunjika kwa kwenda ndani. Aliteremka taratibu mpaka chini ambapo alipumzika kwa msaada wa mikono migumu ya John Murphy. Murphy alimvuta harakaharaka na kumhifadhi nyuma ya lile jiwe kabla ya kumvua nguo na yeye kuzivaa. Alipokamata bunduki yake, G5, Murphy alifurahi. Kwani sasa alikuwa kama mlinzi wa upande wa nje."

    "Vijana wa Tume hawakuwadharau magaidi hata kidogo. Wote walikuwa rasmi katika magwanda ya kijeshi ya EAC, na silaha hatari za daraja la kwanza. Wenzake wawili wakiwa tayari wameshavaa mikanda ya Caliber Sniper na Debbie akijaribisha kunyanyua ya mpenzi wake ili ampe lakini akaiweka chini kwa sababu ya uzito, Murphy na Radia waliweka za kwao mabegani na kuwa tayari kuruka seng’enge. Debbie alicheka kwa kutoamini Murphy alivyonyanyua bunduki yake ya aina yake, ile aliyoshindwa kuibeba, na kuiweka vizuri begani huku akizungusha mkanda wa risasi katika tumbo na kubakiza sehemu ya mbele ambayo hata hivyo aliizungusha katika mkono wake wa kushoto. Bastola, mabomu na visu walivificha ndani ya vijibegi na mikanda ya suti zao za EAC. Radia alikuwa kimya na .50 Caliber Sniper Rifle na bunduki ndogo, G5, yenye shabaha ya hakika na nzuri huenda kuliko zote duniani."

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...