Friday, 12 December 2014

UNSC

UNSC ('United Nations Security Council', Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa) ndiye mmiliki wa WODEC ('World Drugs Enforcement Commission', Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya).

http://www.enockmaregesi.com

2 comments:

  1. WODEA ('World Drugs Enforcement Administration') ni shirika la kujitegemea la kimataifa – linalofanya kazi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa – lenye nia/shabaha ya kukomesha (katika dunia) madawa haramu ya kulevya, ya madaraja yote, pamoja na ugaidi wa kimataifa wa aina zote – hasa wa kimadawa, kisiasa na kinyukilia; kwa ajili ya amani, afya na usalama wa kimataifa. WODEA ilianzishwa chini ya Mkataba wa Kisheria wa Kimataifa wa WODEA ('WODEA Statute') uliosimamiwa kwa kipindi cha siku tatu mfululizo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UNSC, Novemba 1975. Tofauti na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyukilia, IAEA, ambalo huwajibika kwa UNSC na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa; WODEA huwajibika kwa UNSC na Baraza la Uchumi na Ustawi wa Jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC.

    WODEC, Chombo Kikuu cha WODEA, ambayo hutumika kama kongamano la majadiliano ya masuala ya madawa na ugaidi ya kimataifa; huundwa na vyombo vingine vidogo vitatu: Bodi ya Makamishna ya Tume ya Dunia (WBC – 'WODEC Board of Commissioners'), Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia (WGC – 'WODEC General Conference') na Sekretarieti ya Tume ya Dunia. WBC ni Chombo cha Sera cha Tume ya Dunia. Kina wajumbe 12 wanaoteuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na 26 wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia. Wajumbe 12 (watano wa kudumu wa UNSC na saba viongozi wa kanda za WODEA) huteuliwa na UNSC kwa kipindi cha miaka mitano wakati 26 huchaguliwa na WGC kwa kipindi kimoja cha miaka miwili. WBC hutoa mapendekezo kwa WGC kuhusu bajeti na shughuli zote za WODEA.

    Ijue WODEA kupitia hapa; http://enockmaregesi.wordpress.com/wodea/

    ReplyDelete
  2. WODEA ni shirika la kubuni, kwa ajili ya riwaya ya 'Kolonia Santita'.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...