Monday, 16 June 2014

Mafanikio

89. Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote; au 'pushing the envelope' kwa lugha ya kigeni.

http://www.facebook.com/koloniasantita

3 comments:

  1. Kusema hapana kwa ndiyo nyingi ni kutokukubaliana na ushauri wa watu wasiyoijua ndoto yako vizuri. Mfano, kama ndoto yako ni kuwa mchezaji bora wa mpira wa miguu halafu mtu akasema mpira hauna manufaa kwako hata kama ana nia mbaya au njema; eti kitu chenye manufaa kwako labda ni sanaa, sema hapana kwa hiyo ndiyo yake. Kwa sababu ndoto yako unaijua mwenyewe. Neno WOTE katika Falsafa ya Mafanikio ina maana kubwa. Watu wengi hujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao; lakini ukijitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote, utaweza kufanikiwa.

    ReplyDelete
  2. Maana halisi ya falsafa ya 'Sema hapana kwa ndiyo nyingi' ni kutokukubaliana na ushauri wa kila mtu unayekutana naye, maana watu hawaoni kile ambacho wewe unakiona. Kanuni ya mafanikio ni moja isiyobadilika na inayokubalika kila sehemu wakati wowote na kwa watu wote. Ipo mifano mingi ya watu waliofanikiwa kwa juhudi zao wenyewe na ipo mifano mingi ya watu walioshindwa licha ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote, bila kujali maeneo yao ya kijiografia. Tukiacha uvivu wa kufikiri na kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kufuata ushauri wa watu wanaokubaliana na vipaji vyetu, hata Mungu atatusaidia.

    ReplyDelete
  3. Nalazimika kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu ya historia ya maisha yangu.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...