Friday, 16 May 2014

Kisu

Kisu cha kijeshi cha John Murphy alichotumia kumchoma mlinzi wa Panthera Tigrisi Kahima the Warrior kwenye paja – nje ya Bandari ya Salina Cruz huko Oaxaca nchini Meksiko; na alichopendelea kutumia katika sanaa ya mapigano ya Karambiti.

http://www.enockmaregesi.com

3 comments:

  1. Nakumbuka jinsi kahima alivyopiga kelele baada ya murphy kumchoma na kisu!!

    ReplyDelete
  2. hicho ni kisu cha makomandoo wa tume ya dunia.kilamtu kati ya vijana wanne wa tume alikuwa nacho cha kwake pamoja na silaha zingine

    ReplyDelete
  3. "Mikono ya Murphy ikiwa imenasa katika mikono ya Kahima kama ulimbo katika ndege, Murphy aliendelea kujitutumua lakini Kahima akakataa katakata kuruhusu mahuluku mdogo kama yeye kumshinda nguvu. Murphy alikunywa maji na kuhisi kuchanganyikiwa na kuishiwa nguvu. Kabla hajaachia mikono ili azimie, Murphy alikumbuka alikuwa na kisu katika buti ya mguu wake wa kulia; alikichukua. Kwa nguvu zake zote alirusha kisu katika paja la Kahima, Kahima akapiga kelele na kumwachia. Alipoponyoka aliibuka na kuvuta hewa na kuachia pigo jingine la kisu lakini Kahima akawa mjanja. Alidaka mkono wa Murphy, uliokuwa na kisu, na kujaribu kuuvunja kwa hasira. Lakini hakuuvunja. Murphy aliubana lakini Kahima akawa na nguvu nyingi zaidi na kumzamisha tena. Murphy alivyoibuka kwa nguvu za ziada, Kahima akiwa ameng’ang’ania mikono yake yote, aliruka 'hedi'; akampata katika pua, akaruka nyingine na nyingine na nyingine, Kahima akaona maruweruwe na kuachia mkono mmoja. Kisu cha Murphy kikiwa kimeshatumbukia majini, Murphy alisogea nyuma na kuanza kumpigia mahesabu Kahima, akihema mithili ya mbwa." Habari ya kisu cha kijeshi cha John Murphy inapatikana katika ukurasa wa 360 - 361 wa Kolonia Santita.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...