Bastola ya kalamu ya John Murphy Ambilikile aina ya Stinger; iliyotumiwa na
Murphy kumuua kinyama jambazi sugu wa CS-Moscow – Tawi la Kolonia Santita nchini
Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki; na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini
kama vile Masedonia, Montenegro, Uturuki na Ugiriki – Vladimir, huko Yugo
Zapadnaya mjini Moscow, katika dacha ya Kolonia Santita.
http://www.enockmaregesi.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Siku ya kuzaliwa ni siku ya kwanza ya safari nyingine ya siku 365, saa 5, dakika 48, sekunde 46 na maili milioni 600 kulizunguka jua. Safi...
Bastola ya kalamu aina ya Stinger (tamka 'Sting'a') ni silaha 'halali' kwa matumizi ya kawaida ya binadamu huko nchini Marekani hadi hii leo; halali kwa maana ya ATF – Shirika la Pombe, Tumbaku na Silaha la Marekani – kuichukulia kama silaha ya kawaida. Lakini Stinger ya John Murphy haikuwa (wala haijawahi kuwa) silaha ya kawaida! Ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS – 'WODEC Intelligence Services') na kwa ajili ya matumizi ya Kikosi cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC – 'Executive Action Corps'). Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi moja ndogo kwa wakati mmoja – iliyokuwa na ukubwa wa inchi 0.22 ya mtutu wa bunduki ('.22 caliber') – na kidonge kimoja cha 'cyanide' ('potassium suicide pill'): ili akitekwa akimeze na kufa; kuliko kutoboa siri za EAC, na siri za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya. Aidha, Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kufyatua risasi ikiwa imenyooka (Stinger ya kawaida hufyatua risasi ikiwa imejikunja) na kifyatulio chake kilikuwa kwenye kichwa cha kalamu; na ilikuwa na koki mbili: moja kwa ajili ya risasi, na nyingine kwa ajili ya mrija wa kalamu, tofauti na Stinger ya kawaida ambayo ina koki moja, mbele ya kifyatulio. Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kuandika kama kalamu ya kawaida! Ilikuwa na uwezo wa kutumia kiwambo cha kupunguza sauti, kama Stinger za kawaida.
ReplyDelete