Msitu wa Mvua wa Amazoni nchini Kolombia – na nchi zingine nane za kaskazini mwa bara la Amerika ya Kusini huko 'Americas' – magaidi wa Kolonia Santita walipokuwa wameficha tani 600 za madawa ya kulevya chini ya uangalizi wa waasi wa kisiasa wa Kolombia, Peru, Brazili, Venezuela na Bolivia, kabla ya kuzihamishia nchini Meksiko kwa ajili ya usambazaji wa dunia nzima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
120. Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu. http://www.enockmaregesi.wordpress.com
-
157. Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia. http://www.facebook...
Ndani ya kitabu cha 'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi', mtu mwenye historia kubwa na Msitu wa Amazoni ni Nicolas Kahima Kankiriho – mwanajeshi wa kulipwa wa Uganda – aliyetoroka na El Tigre katika nyambizi ya 'Jefe de Jefes' SPD ('the Silent Predator of the Deep'), iliyotengenezwa na Belinsky, katika Ghuba ya Meksiko Septemba 16, 1986. Msitu wa Amazoni ndiyo uliyomkuza Kankiriho, na ndiyo uliyompatia kazi kama mlinzi binafsi wa Kiongozi wa Kolonia Santita.
ReplyDeleteLakini huyu Kahima ni nani? Kahima ('Kahima the Warrior' (kama alivyokuwa akiitwa na makomandoo na wafanyakazi wenzake huko Uganda na Kolombia)); alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Ankole – kusini-magharibi mwa Uganda – Julai 24, 1954, mtoto wa tano kuzaliwa, katika familia ya watoto sita ya Mzee Nicodemas Kankiriho (mzee wa heshima wa Wabaima) aliyekuwa akisifika sana kwa uchungaji wa mifugo na msisitizo mkali wa ukristo kwa watoto wake wote; hususan Kahima na Yebare (1955 – 1978), binti yake wa pekee, aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa.
Baada ya kutoka Uganda – kwa mafunzo ya mwanzo ya ukomandoo ya Kiisraeli – Kahima (futi 6 inchi 3 aliyekuwa akiongea Kinyankole, Kiswahili, Kiingereza na Kihispania kwa ufasaha) alikwenda Urusi na Korea ya Kaskazini, ambako aliongeza ujuzi kwa kiwango cha juu (zaidi) katika medani ya ugaidi wa kisiasa na ukomandoo; kabla ya kwenda Amerika ya Kusini, kama askari wa msituni wa vyama vya kisiasa visivyo rasmi vya 'magorila' wa Kolombia, ndani kabisa ya Msitu wa Amazoni. Akiwa Amazonia, Kahima alikutana na Eduardo Chapa de Christopher (kiongozi wa zamani wa Kateli ya Diablos de Amazonas, Mashetani wa Amazoni, iliyokuwa ikivilinda vyama haramu vya kisiasa vya Amerika ya Kusini) ambaye alimwajiri kama mlinzi binafsi, na baadaye kama mlinzi binafsi wa Carlos Pulencio Alcántara – kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita.
Msitu wa Amazoni ni msitu mkubwa kuliko misitu yote ya mvua ulimwenguni, wenye ukubwa wa kilometa za mraba milioni 5.5 (maili za mraba milioni 2.123), uliotapakaa katika nchi tisa za Amerika ya kusini; ikiwemo Bolivia, Venezuela, Brazili, Peru, na Kolombia.