Nyambizi ya Panthera Tigrisi iitwayo SPD (the Silent Predator of the 
Deep) ikiyoyoma katika Ghuba ya Meksiko; baada ya Panthera Tigrisi 
kutangaza vita na Serikali ya Meksiko Septemba 16, 1986, The People’s Don akiwa 
na makomandoo wake Narochnitskaya Belinsky na Nicolas Kahima Kankiriho (‘Kahima 
the Warrior’) na wanajeshi wengine 17 wa Autodefensa!
http://www.enockmaregesi.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wanauwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya Panthera Tigrisi (El Tigre) ya kubadili katiba ya nchi – kuondoa kipengele cha mkataba wa kubadilishana watuhumiwa na washtakiwa – ili akikamatwa asipelekwe Marekani ambako atafungwa na kufia gerezani, El Tigre aliilaani Serikali ya Meksiko. Kujibu mapigo, ya laana ya maluuni, Serikali ya Meksiko ikawakabidhi makamanda 7 wa Kolonia Santita kwa mamlaka za Marekani, na kuongeza juhudi za kumsaka El Tigre mpaka nje ya Amerika ya Kusini na Kaskazini. El Tigre, kuikomoa serikali na kuwalipia kisasi makamanda wote waliouwawa na kufungwa na shirikisho, akamuua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (PGR) na maafisa 7 wa Jeshi la Polisi la Nchi (PJF) kulinganisha idadi ya makamanda wake waliopelekwa Marekani – halafu 'akapotea', kabisa; baada ya kutangaza vita na Serikali ya Meksiko!
ReplyDeleteTume ya Dunia imekuwa ikimtafuta Chui wa Siberia kwa zaidi ya miaka tisa. Bila mafanikio. Ulinzi wa Panthera Tigrisi ni wa kimataifa. Mbali na kulindwa na wananchi wa Oaxaca (kwa sababu ya kuwajengea shule, hospitali, makanisa, na kadhalika), na polisi wa shirikisho (kwa sababu ya vitisho, mauaji na rushwa); El Tigre analindwa na jeshi binafsi la kujihami (autodefensa) la wanajeshi wastaafu zaidi ya 1300! Mbali hali kadhalika na autodefensa; kiongozi wa Kolonia Santita ana walinzi binafsi makomandoo (48) akiwemo A. Narochnitskaya Belinsky, mtaalamu wa kutengeneza nyambizi wa Urusi, na Nicolas Kahima Kankiriho ('Kahima the Warrior') mwanajeshi wa kulipwa wa Uganda – aliyetoroka na El Tigre katika nyambizi ya Jefe de Jefes SPD ('the Silent Predator of the Deep'), iliyotengenezwa na Belinsky, katika Ghuba ya Meksiko Septemba 16, 1986.