Wednesday, 8 January 2014

Kitendawili 1

JIBU LA KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA

Swali:

Kila namba kati ya namba zifuatazo ina maana kubwa katika kitabu cha Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi, kuanzia na jalada la mbele. Tegua (kokotoa) kitendawili cha Kolonia Santita.

Msimbo:

35 - 12 - 4 - 2 - 88

Jibu:

Katika jalada la mbele la kitabu cha Kolonia Santita kuna maneno 12 na herufi 82 na nafasi 8 miongoni mwa hayo maneno 12. Kuna jumla ya herufi 90. Ukiziba myanya yote ya picha kuu ya biohazard ya kitabu utapata 88.

90 ÷ 12 = 7.5

7.5 hapa ni kiashirio (symbolic). Na nukta (.) katika elimu ya hesabu ni sawa na alama ya kuzidisha. Kwa kutumia kanuni ya kawaida ya sayansi ya namba:

7 x 5 = 35

7 + 5 = 12

7 ÷ 5 = 4

7 – 5 = 2

35 + 12 + 4 + 2 = 53

53 + 35 = 88

88 inalingana (corresponds) na 88 ya picha ya kitabu ya tahadhari ya kibiolojia ya biohazard. Inawakilisha maneno yote ya jalada la mbele la kitabu cha Kolonia Santita.

Hivyo?

35 – Inawakilisha umri wa Frederik Mogens na imedhihirishwa katika ukurasa wa 113 wa Kolonia  Santita.

12 – Inawakilisha umri wa Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia cha Executive 
Action Corps. EAC ilianzishwa mwaka 1980. Imedhihirishwa katika ukurasa wa 12 wa Kolonia 
Santita.

4 – Inawakilisha Vijana wa Tume. Imedhihirishwa katika faslu ya pili ya sura ya kwanza ya Kolonia Santita.

2 – Inawakilisha Tume ya Dunia na Kolonia Santita – vikundi viwili vinavyopingana katika riwaya ya Kolonia Santita.

88 – Inawakilisha namba ya bahati ya Meja John Murphy Ambilikile na alama ya udhalimu ya Kolonia Santita. Namba ya bahati ya John Murphy imedhihirishwa katika ukurasa wa 163 wa Kolonia Santita. Alama ya udhalimu ya Kolonia Santita imedhihirishwa katika picha ya kitabu (picha kuu) cha Kolonia Santita ya biohazard.

Hitimisho:

Maneno ya jalada la mbele la kitabu cha Kolonia Santita yameunganishwa kimantiki na picha za kitabu ambazo zimeunganishwa kimantiki na salio la kitabu kizima.

www.enockmaregesi.com | www.enockmaregesi.org
 

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...