61. Kuandika hadithi ni kitu kimoja. Kuweka kanuni za fasihi katika hadithi ni kitu kingine.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
120. Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu. http://www.enockmaregesi.wordpress.com
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
Msomaji wa kawaida wa hadithi au maandiko yoyote hajali iwapo anachokisoma kimeandikwa kwa utaalamu au la – hakuna atakayejali iwapo kanuni za fasihi zitavunjwa ili kupendezesha hadithi au maandiko yoyote. Wengi wanachojali ni utamu wa hadithi wanayoisoma, si kanuni za fasihi zilizotumika katika maandalizi ya hadithi hiyo. Lakini hayo yanaweza kusamehewa. Kisichoweza kusamehewa ni tahajia, sarufi au matumizi ya mazungumzo ya kawaida ya mtaani katika maandiko ya hadithi.
ReplyDeleteKanuni maarufu katika fasihi ni "Onesha, usiambie". Ukisema "John alikuwa na furaha," unamtaarifu msomaji kwamba John alikuwa na furaha. Lakini ukisema "John alitabasamu," unampa msomaji akili itakayofanya ajue kama John alikuwa na furaha. Unamwonesha, humwambii! Kanuni hii ni nzuri katika fasihi na ndivyo mambo yalivyo katika maisha ya kila siku. Kama John ni mfanyakazi mwenzako, hatuna mtu wa kutuambia kama John ana furaha kwa sababu ya kupandishwa cheo au mshahara. Tunachotakiwa kufanya ni kuchunguza vizuri tabia ya John na kujua nini kinaendelea katika maisha yake. Kuonesha humfanya msomaji azame katika hadithi – hufanya hadithi ionekane ya kweli – hasa mwandishi anapounganisha vyema ubunifu na uhalisia.
Kanuni za fasihi ndiyo msingi wa maandiko yote ya kitaalamu hapa ulimwenguni. Watu hawana budi kuzifuata kanuni hizo iwapo wanataka kutumia vipaji vyao katika ngazi ya kimataifa.