WODEA (World Drugs Enforcement Administration) ni shirika la kujitegemea la kimataifa – linalofanya kazi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa – lenye nia/shabaha ya kukomesha (katika dunia) madawa haramu ya kulevya, ya madaraja yote, pamoja na ugaidi wa kimataifa wa aina zote – hasa wa kimadawa, kisiasa na kinyukilia; kwa ajili ya amani, afya na usalama wa kimataifa. WODEA ilianzishwa chini ya Mkataba wa Kisheria wa Kimataifa wa WODEA (WODEA Statute) uliosimamiwa kwa kipindi cha siku tatu mfululizo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC Novemba 1975. Tofauti na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyukilia, IAEA, ambalo huwajibika kwa UNSC na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa; WODEA huwajibika kwa UNSC na Baraza la Uchumi na Ustawi wa Jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC.
WODEC, Chombo Kikuu cha WODEA, ambayo hutumika kama kongamano la majadiliano ya masuala ya madawa na ugaidi ya kimataifa; huundwa na vyombo vingine vidogo vitatu: Bodi ya Makamishna ya Tume ya Dunia (WBC – WODEC Board of Commissioners), Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia (WGC – WODEC General Conference) na Sekretarieti ya Tume ya Dunia. WBC ni Chombo cha Sera cha Tume ya Dunia. Kina wajumbe 12 wanaoteuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na 26 wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia. Wajumbe 12 (watano wa kudumu wa UNSC na saba viongozi wa kanda za WODEA) huteuliwa na UNSC kwa kipindi cha miaka mitano wakati 26 huchaguliwa na WGC kwa kipindi kimoja cha miaka miwili. WBC hutoa mapendekezo kwa WGC kuhusu bajeti na shughuli zote za WODEA.
Rais wa WODEA huchaguliwa na WGC kwa mapendekezo ya UNSC. WBC hupendekeza majina sita kwa UNSC ambayo huchagua majina matatu kati ya hayo sita na kuyapeleka katika Mkutano Mkuu wa WODEA – kupigiwa kura ya Kamishna Mkuu wa WODEC na Rais wa WODEA kwa kipindi cha miaka mitano. Kamishna Mkuu wa WODEC ni Rais wa WODEA. Wakati WBC hukutana mara nne kwa mwaka mjini Copenhagen kuanzia Novemba, WGC (nchi wanachama 143) hukutana mara moja kwa mwaka katika mwezi wa Novemba kuidhinisha bajeti na mapendekezo ya WBC – kwa ajili ya Sekretarieti ya Tume ya Dunia. 
Sekretarieti ya Tume ya Dunia huwajibika na utekelezaji wa mapendekezo yote yaliyopitishwa na WBC na WGC kwa niaba ya WODEA. Huchaguliwa na WBC na kuidhinishwa na WGC kwa kipindi cha marudio cha miaka mitano. Sekretarieti ya Tume ya Dunia huwajibika pia na nguvukazi ya watu zaidi ya 7,000 duniani kote na bajeti ya wastani wa dola za kimarekani milioni 400 kwa kwaka mzima.
Mbali na WBC, WGC na Sekretarieti ya Tume ya Dunia, WODEC ina vyombo vikubwa vitatu vya dola: Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia (WPD), Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS) na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC). EAC iliundwa kwa makubaliano maalumu ya Azimio la Copenhagen kati ya WODEA na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa – Novemba 1980. 
WODEC ina maabara tatu za kikemia, ofisi tatu za mahusiano mema (Vienna, Pretoria na New York), kliniki saba za madawa ya kulevya na kanda sita katika mabara sita ya dunia nzima. Kila kanda ina bodi ya wakurugenzi, idara ya polisi, usalama, sekretarieti, maabara na kliniki za madawa ya kulevya. Kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia huanzia Somalia mpaka Kameruni mpaka Afrika Kusini. Kanda ya Afrika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia huanzia Eritirea mpaka Nijeria mpaka Tunisia, isipokuwa Moroko ambayo iko katika kanda ya Ulaya.
enockmaregesi.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 
That is history of WODEA - UN fictional agency on drugs and nuclear materials.
ReplyDeleteWODEA is a fictional independent international agency; employed by the United Nations to bring peace, security and prosperity to the world by fighting illegal drugs; and narco, political and nuclear terrorism. WODEA is independent of the control of the UN General Secretary. WODEA ni shirika la kubuni la kujitegemea la kimataifa – linalofanya kazi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa – lenye lengo/kusudi la kudhibiti ( katika dunia) madawa haramu ya kulevya ya madaraja yote, pamoja na ugaidi wa kimataifa wa aina zote – hasa wa kimadawa, kisiasa na kinyukilia; kwa ajili ya amani, afya na usalama wa kimataifa.
ReplyDelete