Tuesday, 19 February 2013

EAC

Executive Action Corps (au EAC kwa kifupi) ni kitengo chenye wanajeshi bora na mahodari kuliko wote wa Umoja wa Mataifa. Kinaundwa na wanajeshi mahiri 95 (na mbwa 17) wenye sifa maalumu, majina bandia na uwezo wa kijeshi wa kipekee uliotukuka. Sifa za kujiunga na kitengo hiki, chenye kambi yake nje ya Oslo, Norwe; karibu na ofisi za WODEC-Intelligence, kadhalika, ni za kipekee. Nchi yako lazima iwe mwanachama wa Umoja wa Mataifa na mwanachama wa Tume ya Dunia. Lazima, mbali na sifa za kawaida za kiueledi, kijamii na kitaaluma: uwe na sifa nzuri katika jamii. Uwe jasusi mwaminifu wa nchi yako; uwe na shahada angalau moja ya miaka minne ya chuo kikuu; uwe na mkanda mweusi wa sanaa yoyote ya mapigano; uwe na uwezo wa kuongea lugha mbili au zaidi za kimataifa kwa ufasaha; uwe komandoo kamili wa jeshi, mwenye uwezo madhubuti wa kupigana angani, majini na nchi kavu na uwe na Stashahada ya Mchanganuo wa Welekevu wa Kihalifu (Criminal Intelligence Analysis) inayotolewa na Tume ya Dunia peke yake. Hiki ni kikosi maalumu cha kikomandoo cha Tume ya Dunia. Wanajeshi wake hawachaguliwi kwa njia za kawaida za utumaji wa barua za maombi. Wanapendekezwa na Kamati ya Usalama ya Tume ya Dunia na kuteuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

enockmaregesi.com

2 comments:

  1. That is history of EAC (Executive Action Corps) - WODEA's special military force.

    ReplyDelete
  2. Kikosi maalumu cha kikomandoo cha Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya WODEC chenye kambi yake nje ya Oslo nchini Norwe. EAC haina tofauti yoyote na SAS ya Uingereza na Navy SEALs ya Marekani, au Department V ya KGB na Kidon ya Mossad. Huundwa na wanachama zaidi ya 95 (wenye sifa maalumu) waliopendekezwa kutoka nchi-wanachama 143 za Tume ya Dunia, na kuteuliwa kwa kiapo maalumu na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...