Usipojisajili BASATA watasema una kiburi. Serikali hupenda watu iliyoridhika nao. Wasanii wote nendeni BASATA mkajisajili.
BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa) hawataweza kukutambua kwa sababu hujajisajili kwao, na kushirikiana na msanii ambaye hajajisajili BASATA ni kinyume cha sheria.
Kupeperusha bendera ya taifa kwa niaba ya taifa bila kujisajili serikalini ni kosa la jinai, na serikali haitakutambua kwa sababu wewe mwenyewe hujajitambua.
Mambo madogomadogo yanayohusu serikali si ya kudharau. Kama unavyoona umuhimu kukata leseni ya gari lako, ona umuhimu hivyohivyo kujisajili serikalini.
Unataka kuondoa dhambi lakini hukutani na wenye dhambi. Hiyo dhambi utaiondoaje?
Kazi yenu kwetu ni kutusaidia, na kazi yetu kwenu ni kuwasaidia pia; kwani kila mwananchi anao wajibu wa kuisaidia serikali yake. BASATA, katika jina la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, endeleeni kuhamasisha na kuhakikisha wasanii wote nchini wanajisajili; kwa kuendelea kutoa tuzo mbalimbali za sanaa na jitihada nyingine, na kwa kuendelea kufuatilia kuhakikisha kuwa kila msanii anajisajili na kupata kibali.
TRA wanahamasisha na kufuatilia watu walipe kodi. BASATA hamasisheni na kufuatilia wasanii wajisajili.
Kujisajili ni lazima kwa mujibu wa sheria, lakini si kila msanii ambaye hajajisajili BASATA anajua kuwa anafanya kosa.
Kwa pamoja tuijenge nchi yetu.
No comments:
Post a Comment