Monday, 25 December 2017

Ndani na Nje ya Ufahamu Wako

257. Jambo linalofanyika ndani ya ufahamu wako ni lako, lakini lile linalofanyika nje ya ufahamu wako ni la Mungu.

Ukiomba jambo kwa Mungu ukiwa na imani uhitaji kuomba tena. Mungu amekusikia. Jibu lako litafika kama mwizi! Kama Yesu atavyorudi kwa mara ya pili, bila mtu yeyote kujua, ndivyo baraka yako itakavyofika.

Mathalani unaweza kuwa umetuma barua ya maombi ya kazi hadi ukasahau kama waliipata! Kama hiyo kazi ni yako, siku utakapopata barua ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano utakuwa umejisahau! Ukienda kwenye mahojiano utakuwa na nafasi kubwa mno ya kupata hiyo kazi! Lakini ukikumbuka kwamba ulituma barua ya maombi huku ukifungua akaunti yako ya baruapepe, ukitegemea kukuta barua ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano na kweli ukaikuta, nafasi ya kupata hiyo kazi ni ndogo mno!

Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo (Mithali 25:2). Mungu hupenda kufanya mambo yake kwa siri.

Ukiomba kitu kwa Mungu mwachie Mungu akusaidie yeye mwenyewe kukifikiria! Ukitaka Mungu akukumbuke, jisahau! Hutajua baraka yako itafika lini!

1 comment:

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...