Monday, 18 September 2017

Utajiri Hujulikana kwa Kuwaletea Watu Faraja

243. Utajiri hujulikana kwa kuwaletea watu faraja, na umaskini hujulikana kwa kuwaletea watu taabu.

Umaskini ni mbaya kwa afya yako. Hata kama wewe ni tajiri, maskini au mtu yeyote anayeshi katikati ya makundi hayo mawili, umaskini ni jambo baya kuliko yote katika maisha yako. Kwani Mungu hakukuumba kuwa maskini. Alikuumba kuwa tajiri.

Heri kuwa tajiri wa moyo kuliko kuwa tajiri wa pesa au mali. Ukiwa tajiri wa moyo utaishi mbinguni duniani, utajua chanzo cha matatizo yako yote na utajua jinsi ya kuyatatua, mwili wako utakuwa kama shati ambalo litaweza kubadilishwa muda wowote litakapochakaa. Ukiwa tajiri wa pesa au mali bila kuwa tajiri wa moyo, utakufa maskini.

Tajiri wa moyo ni yule anayejua yeye ni nani na kwa nini yuko hapa. Usikate tamaa, utajiri humpendelea anayejaribu.

1 comment:

  1. Mungu hakumuumba mtu ili awe maskini. Ni dhambi zetu ndizo zinazosababisha tuwe maskini.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...