Friday, 4 August 2017

Ndege ya Shirika la Ndege la Tailandi

Ndege ya Shirika la Ndege la Tailandi, Thai Airways, Airbus A330-321, iliyombeba Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia Meja Jenerali U Nanda wa Bama, kutoka Bangkok mpaka Amsterdam na kutoka Amsterdam mpaka Bangkok; kwenda na kutoka Copenhagen katika Kikao cha Dharura cha Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.

Kwa sababu ya umbali na kwa sababu ya tofauti ya kanda za saa za kanda sita za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (WODEC), Murillo Montana na U Nanda walipewa kipaumbele cha kwanza na Ofisi ya Tume ya Oslo wakati wa kutuma faksi za makamishna za wito wa Copenhagen.

Faksi za Mafuru, Cashman, Kashoggi na Ortega zilitumwa saa nane mchana wa Jumatano. Za Montana na Nanda zilitumwa saa saba mchana, ili ya Montana ifike saa moja asubuhi (Jumatano) na ya Nanda ifike saa kumi na mbili na nusu jioni (Jumatano hiyohiyo), ili wachukue ndege haraka kuwahi kikao Alhamisi saa 11:30 juu ya alama alasiri.

Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia Kamishna Meja Jenerali U Nanda wa Bama (msaliti wa KGB katika miaka ya sitini na mpiganaji namba moja wa vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa sababu ya watoto wake wapendwa Ma Nang Nyi na Ko San Pe); akiwa amepumzika nyumbani kwake Rangoon, Bama, baada ya mazoezi ya jioni Jumatano moja tulivu, Saw Saya – Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia – alikaribishwa katika chumba cha wageni cha nyumba ya kamishna na kuongea na mke wa kamishna Aung Phyu, kabla ya kuongea na kamishna mwenyewe.

Saya alimletea kamishna faksi ya wito na tiketi ya ndege ya Copenhagen, ambapo saa 1:45 jioni aliondoka kuelekea Denmaki.

Kiongozi wa Kanda ya Ulaya ya Tume ya Dunia Miranda Cashman OBE, ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika Copenhagen katika Kikao cha Dharura cha Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya. Alifika saa 6:50 mchana na BA kutokea London, Uingereza. U Nanda alikuwa wa mwisho kufika Copenhagen. Alifika saa 11:20 alasiri na KLM kutokea Amsterdam, hivyo akachelewa kikao.

No comments:

Post a Comment

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...