Monday, 15 May 2017

Segula: Hazina Maalumu ya Mungu

225. Mitume wa Yesu Kristo wakati wanahubiri injili hawakuwa na Roho Mtakatifu, walikuwa hata bado hawajaongoka, lakini walikuwa na idhini maalumu kutoka kwa Mungu ya kuhubiri Neno la Mungu. Neno la Mungu halihubiriwi kwa nguvu zetu sisi wenyewe bali linahubiriwa kwa nguvu za Mungu kutokana na utii kwa uongozi wake.

Iwapo watu watakwenda nje ya kusudi la Mungu, hata wawe makini kiasi gani na injili, maneno yao hata yawe ya hekima kiasi gani hayatawasaidia chochote.

Utii kwa Mungu unapokosekana injili ambayo Mungu anataka ihubiriwe haitahubiriwa. Itahubiriwa na manabii wa uongo.

Mitume wa Yesu Kristo hawakuwa na Roho Mtakatifu lakini walikuwa na kitu ndani cha kiroho zaidi kilichowatofautisha na wengine kwa namna ya kipekee. Walikuwa na segula, walikuwa na haki ya kuwa watoto watakatifu wa Mungu.

Segula maana yake ni hazina maalumu ya Mungu.

Kuna watoto wa Mungu na kuna watoto watakatifu wa Mungu. Watoto wa Mungu ni wale waliobatizwa na kumkaribisha Kristo kama kiongozi wa maisha yao, na hata wale ambao hawajabatizwa na kumkaribisha Yesu kama kiongozi wa maisha yao kwa maana ya uumbaji, wakati watoto watakatifu wa Mungu ni mitume na manabii wa kweli.

Jukumu la kwanza la kanisa ni kueneza injili duniani kote kama tunavyoambiwa katika mathayo 24:14. Haijalishi utaieneza vipi, kwa sababu Mungu hajasema tuieneze vipi. Lakini la kwanza kabisa ni kuwa kwanza mwaminifu kwa Mungu kuweza kueneza injili duniani kote.

1 comment:

  1. Manabii wa uongo wana dhambi kuu tatu: tamaa ya ngono, uasi dhidi ya mamlaka ya Kristo, na dharau kwa Shetani. Nabii wa uongo atampinga Shetani kwa nguvu zake zote, atakuwa na tamaa ya wanawake au wanaume kama ilivyokuwa kwa Sodoma na Gomora na miji yote iliyoizunguka miji hiyo, na atayadharau mamlaka ya Kristo.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...