Wednesday, 4 January 2017
Mungu Hutumia Watu ‘Wajinga’ na ‘Wapumbavu’ Kufanya Mambo Makubwa Katika Maisha Yao na ya Watu Wengine
Mungu hutumia
watu ‘wajinga’ na ‘wapumbavu’ kufanya mambo makubwa katika maisha yao na
ya watu wengine. Katika Biblia, Musa aliitwa mjinga alipokiuka amri ya
Farao ya kuendelea kuwafanya watumwa wana wa Israeli nchini Misri; Nuhu
aliitwa mpumbavu alipohubiri kwa miaka mia kuhusu gharika, katika
kipindi ambacho watu hawakujua mvua ni nini; Daudi aliitwa mjinga
alipojitolea kupambana na Goliati bonge la mtu, shujaa wa Gathi; Yusufu
aliitwa mjinga alipokataa kulala na mke wa bosi wake, baada ya kuwa
ameuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri; Abrahamu aliitwa mjinga
alipoamua kuhama nchi aliyoipenda na kwenda katika nchi ya ahadi, eti
kwa sababu Mungu alimwambia kufanya hivyo; Yesu aliitwa mjinga mpaka
akasulubiwa aliposema yeye ni Mfalme na Mwana wa Mungu. LAKINI, Musa
alitenganisha Bahari ya Shamu na kuwapeleka Waisraeli katika nchi ya
ahadi, ambako aliwakomboa kutoka utumwani. Nuhu aliokoa dunia. Daudi
alimshinda Goliati. Yusufu aliokoa familia yake kutokana na njaa.
Abrahamu alikuwa baba wa imani. Yesu aliyashinda mauti. Wakati mwingine
tunatakiwa kufanya mambo makubwa kulingana na jinsi Roho Mtakatifu
anavyotutuma, bila kujali watu au dunia itasemaje.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...

Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawapaswi kuingilia mambo yako bila idhini ya Mwenyezi Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu.
ReplyDeleteJishushe.
ReplyDeleteShuka kama hayo maneno yalivyoshuka.
ReplyDelete