189. Siri ya utajiri ni mawazo ya mtu. Maisha unayoishi uliyataka
mwenyewe. Amka uishi. Hii ndiyo siri kubwa ya utajiri kuliko zote
ulimwenguni. Ukifikiria chanya maisha yako yatakuwa chanya, ukifikiria
hasi maisha yako yatakuwa hasi. Unachofikiria ndicho unachokuwa. Siri ya
mafanikio yako ni jumla ya mambo unayoyawaza.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...
Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO.
ReplyDeleteKitu cha kwanza jiulize unataka nini. Halafu omba, kwa mungu yoyote unayemwamini. Kisha amini, kwamba umepata, hadi utakapopata.
ReplyDeleteUkifuata kanuni ya nguvu ya uvutano uhitaji kujua jinsi utakavyofanikiwa. Kazi yako ni kuwaza tu kwa namna inavyotakiwa. Waza na amini kwa asilimia 100. Mengine yote mwachie Mungu au ulimwengu. Mungu pekee ndiye anayekupa njia na bahati, ili wewe ufanikiwe. Atakupa nguvu ya kufanya kazi na ujanja wowote utakaohitajika, katika harakati hizo za mafanikio yako.
ReplyDeleteUkiwaza kwa kufuata kanuni ya nguvu ya uvutano (ambayo ni kuwaza na kuamini kama kile unachokiwaza tayari umeshakipata bila hata kujua umekipataje) utaishi kama ulivyowaza. Ukiwaza kuwa jambazi utakuwa jambazi hakika, ukiwaza kupona ugonjwa unaokusumbua utapona hakika, na ukiwaza kuwa tajiri utakuwa tajiri hakika. Mafanikio hayo yanaweza kuchukua mwezi mmoja kutimia au yanaweza kuchukua miaka kumi. Unachotakiwa kufanya ni kuwaza na kuamini.
ReplyDelete