Monday, 15 August 2016

Mtoto Mchanga

186. Kwa nini mtoto mchanga anapokuwa ananyonya ziwa la mama yake, mara nyingi humwangalia mama yake machoni? Kwa sababu, licha ya macho kuonekana kitu cha ajabu kwake, mtoto mchanga, bila kujitambua, hutamani sana mama yake amwambie neno zuri atakalolitumia baadaye katika maisha yake atakapokuwa mkubwa. Maneno huumba. Ukimwambia mwanao kuwa anaonekana atakuwa jambazi, anaweza kuwa jambazi kweli atakapokuwa mkubwa; ukimwambia kuwa anaonekana atakuwa mwanasheria, anaweza kuwa mwanasheria kweli atakapokuwa mkubwa.

http://www.facebook.com/koloniasantita 

2 comments:

  1. Watoto hupenda vitu vinavyong’aa ambavyo havijatulia na vilivyopangiliwa vizuri. Hivyo ndivyo macho ya binadamu yalivyo: yana unyevu na yanaakisi mwanga, hayajatulia, na yana rangi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na kope na vigubiko vya macho ambavyo pia hazijatulia. Mtoto mchanga hasa yule anayeona vizuri huangalia macho pale anapopata nafasi, kwa maana ya kuyashangaa. Vilevile, huangalia macho kwa maana ya kupokea molekuli ya maadili au homoni inayorahisisha maisha kutoka kwa mama yake iitwayo ‘oxytocin’. ‘Oxytocin’ husisimua ubongo wake na kuutayarisha kupokea neno lolote litakalosemwa na mama yake mzazi au mama yake mlezi.

    Jicho ni kiungo cha ajabu zaidi kuliko viungo vyote katika mwili wa mwanadamu baada ya ubongo. Jicho moja linatengenezwa na viungo vidogovidogo zaidi ya milioni mbili, vinavyofanya kazi kwa pamoja bila kukosea. Macho yana nguvu ya ajabu. Huu ni wito kwa akina mama wanaonyonyesha: Usizungumze maneno mabaya mtoto wako mchanga anapokuangalia machoni wakati ananyonya ziwa lako. Neno lolote utakalomwambia, zuri au baya, pamoja na kwamba amekuwa akisikia sauti yako kwa miezi kadhaa akiwa tumboni, litajirekodi katika akili yake isiyotambua bila wewe au yeye mwenyewe kujua. Neno hilo litakuja kumuathiri baadaye atakapokuwa mkubwa. Atakapopevuka, atakapokuwa na uwezo wa kupambanua mambo, atakuwa anaota na kuwaza kile ambacho ulikuwa ukimwambia alipokuwa tumboni; na alipokuwa akinyonya na kukukodolea macho.

    Kama ulikuwa ukimwambia mwanao kuwa atakuwa jambazi labda kwa sababu ya fujo zake alipokuwa mdogo, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota atakapopevuka akili ni ya kihalifu. Kwani hayo ndiyo mambo ya kwanza kabisa kujirekodi katika ubongo wake alipokuwa hajitambui. Lakini kama ulikuwa ukimwambia kuwa atakuwa daktari au mwanasheria, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota ni ya kidaktari au kisheria. Kuna uwezekano mkubwa akawa daktari au mwanasheria baadaye katika maisha yake.

    Mwambie mtoto wako maneno mazuri anapokuwa ananyonya na kukuangalia machoni kwa kukukodolea. Maneno utakayomwambia ndiyo yatakayokuwa msingi wa mawazo yake, na ndiyo yatakayoumba maisha yake atakapokuwa mkubwa.

    Tengeneza maisha ya mwanao kwa kuongea naye maneno mazuri anapokuwa tumboni mwako, na anapokuwa ananyonya akikuangalia machoni.

    Mtoto asipokuangalia machoni wakati ananyonya anaweza kuwa na matatizo ya akili. Heri kumwona daktari mapema.

    ReplyDelete
  2. Mwenye akili atajua aongee nini na mtoto wake. Si mtoto mchanga tu, hatua zote za utoto.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...