Monday, 25 April 2016

Shetani

170. Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.

http://www.facebook.com/koloniasantita

4 comments:

  1. Kuna vitu vitatu ndani ya mtu: kuna hiari, kuna ufahamu, na kuna mwili. Hiari inatawaliwa na Mungu; ufahamu unatawaliwa na malaika mwema; mwili unatawaliwa na nyota lakini chini ya usimamizi wa malaika wema: malaika wema walisimamisha jua na mwezi kwa ajili ya Yoshua na wana wa Israeli juu ya Gibeoni na katika bonde la Aiyaloni, walirudisha jua nyuma kwa ajili ya Hezekia mfalme wa Yuda na kwa ajili ya nabii Isaya, na waliifanya dunia ‘kuvaa koti’ ghafla wakati wa kusulubiwa kwa Mwanakondoo wa Mungu Anayeondoa Dhambi. Moyoni ni mahali patakatifu. Hata malaika wema hawawezi kuona ndani ya moyo wa mtu, ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya hivyo, na alichokihifadhi Mungu ndani ya moyo huo ni hiari ya mtu ya kuchagua mema au mabaya.

    ReplyDelete
  2. “Kutakuwepo na nguvu za chanya na hasi katika maisha yako kadiri utavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu moyo wako kuwa chanya utakuwa chanya. Ukiruhusu moyo wako kuwa hasi utakuwa hasi. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako mpaka wewe mwenyewe umwoneshe. Ukionesha chanya Mungu atakupa chanya. Ukionesha hasi Shetani atakupa hasi.” – Enock Maregesi

    ReplyDelete
  3. Shetani hana uwezo wa kupandikiza chuki au upendo au kitu chochote ndani ya moyo wa mtu, bila mtu mwenyewe kupenda.

    ReplyDelete
  4. Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, binadamu angeshatengeneza moyo.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...