Monday, 4 April 2016

Aliyekupandisha

167. Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu.

http://www.facebook.com/koloniasantita

2 comments:

  1. Usimdharau mtu aliyesaidia kukusukuma juu katika ngazi ya mafanikio yako, ikiwa utafanikiwa, kwa sababu kuna leo na kesho. Ukishuka, kama ulimdharau, hatakuamini tena. Lakini ukishuka, kama ulimheshimu, na kama bado ana uwezo wa kukupandisha juu, atakupandisha tena.

    ReplyDelete
  2. Usimdharau mtu aliyesaidia kukupa kazi ulipokuwa huna kazi, wala usimdharau mtu aliyesaidia kukulea ulipokuwa mdogo, au mtu aliyeokoa maisha yako au mtu aliyekusaidia kwa namna yoyote ile. Ukimdharau, utakaposhuka, atakusaidia kwa rehema za Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...