158. Kuna mafanikio ya aina mbili hapa duniani: Mafanikio ya Shetani na
mafanikio ya Mungu. Mafanikio ya Shetani ni rahisi kupata na ni ya
kitumwa. Mafanikio ya Mungu ni magumu kupata lakini ni ya hakika. Mungu
akikubariki, pesa inaongezeka kama inavyoongezeka saa.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...
Ukiwa na mafanikio ya Shetani hayo si mafanikio ya kweli. Ukiwa na mafanikio ya Mungu hayo ndiyo mafanikio ya kweli. Mafanikio ya kweli hayatokani na NINI unacho. Mafanikio ya kweli yanatokana na NANI unaye. Yesu Kristo alikuwa maskini, hakuwa na kitu; lakini alikuwa tajiri, alikuwa na Mungu ndani ya moyo wake.
ReplyDelete"Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu." –Enock Maregesi
ReplyDeleteYusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi.
ReplyDelete