Monday, 22 February 2016

Mimi

161. Hakuna mimi katika umoja. Kuna sisi.

http://www.facebook.com/koloniasantita

4 comments:

  1. Katika umoja hakuna 'umimi', kuna 'sisi kwa pamoja'; na lengo la umoja ni kutengeneza nguvu, ya ziada.

    ReplyDelete
  2. "Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano." –Enock Maregesi

    ReplyDelete
  3. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi (ubinadamu), si mimi (ubinafsi). Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano watakuwa na nguvu ya watu watano! Watakuwa na nguvu ya ziada kufanikisha malengo kama vile kuwa na uwezo wa kusaidia jamii kama timu au kama mtu binafsi, kujenga jengo la ofisi, kutengeneza ziada katika masuala ya uchumi wa kampuni au nchi au wa mtu binafsi, ushindi katika kitu chochote kile, na kadhalika. Mimi ni ubinafsi. Sisi ni ubinadamu. Ubinafsi ni uvivu. Ubinadamu ni uchapakazi.

    ReplyDelete
  4. Usifanye kazi peke yako wala usiwe mbinafsi! Washirikishe wenzako kukamilisha malengo madhukura ya kadari ya maisha yako.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...