Monday, 6 July 2015

Chanya

144. Kutakuwepo na nguvu za chanya na hasi katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu moyo wako kuwa chanya utakuwa chanya. Ukiruhusu moyo wako kuwa hasi utakuwa hasi. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako mpaka wewe mwenyewe umwonyeshe. Ukionyesha chanya Mungu atakupa chanya. Ukionyesha hasi Shetani atakupa hasi.

http://www.facebook.com/koloniasantita

2 comments:

  1. Shetani alikuwa malaika aliyeumbwa na Mungu lakini baadaye akamwonea Mungu wivu, wivu wa madaraka, hivyo Mungu akamtupa duniani kwa sababu ya kupingana na utawala wake mtakatifu. Duniani Shetani akamtumia nyoka kama mdakale kumdanganya Hawa. Hawa na Adamu wakamsikiliza Shetani badala ya kumsikiliza Mungu, nao wakalaaniwa. Shetani akajidai kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya uzao wote wa Adamu na Hawa uwe mbali na Mungu, hivyo Mungu akampa muda wa kujaribu na kuthibitisha madai yake, lakini Shetani mpaka leo bado hajafanikiwa. Wakiitawala dunia leo kwa udanganyifu wa hali ya juu, pamoja naye, ni baadhi ya malaika ambao Shetani alifanikiwa kuwalaghai huko mbinguni. Mungu akawalaani pia na kuwatupa huku duniani, ambako Shetani alipapenda zaidi.

    Kutakuwepo na nguvu za hasi na chanya katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na hasi utakuwa hasi. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na chanya utakuwa chanya. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako hadi wewe wenyewe umwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya uzinzi atakupa uzinzi. Ukionyesha tamaa ya ulevi atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi atakupa wizi, na kadhalika. Kadiri utavyojitahidi kuwa chanya ndivyo utakavyozidi kuwa chanya; na kadiri utavyojitahidi kuwa hasi ndivyo utakavyozidi kuwa hasi. Usipambane na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo.

    Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii.

    ReplyDelete
  2. Nguvu za hasi ni mawazo mabaya, na nguvu za chanya ni mawazo mazuri. Nguvu za hasi ni Shetani, kwa vile Shetani ndiye anayeleta mabaya. Nguvu za chanya ni Mungu, kwa vile Mungu ndiye anayeleta mazuri. Katika dunia hii utapambana na Shetani lakini hutamshinda, kwani hapa ndipo anapotawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho, kwa maana ya maombi na utiifu kamili kwa Mwenyezi Mungu, kama unataka kuzishinda nguvu zake.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...