143. Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume.
ReplyDeleteNatafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema – sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu.
ReplyDeleteSina nyemi na mwanamke mwenye sura nzuri na tabia mbaya. Nina nyemi na mwanamke mwenye sura mbaya na tabia nzuri, au mwanamke mwenye sura nzuri na tabia nzuri. Mwanamke wa kuoa sitampenda nitampendelea.
ReplyDeleteHakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
ReplyDelete