http://www.enockmaregesi.wordpress.com
Thursday, 21 May 2015
M16
http://www.enockmaregesi.wordpress.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

Bila bunduki ya M16 John Murphy huenda angeuwawa na magaidi huko Xochimilco ('Sochimiliko'), karibu na sanamu la karne ya kumi na sita la 'Parroquia de San Bernardino de Siena' jijini Mexico City, baada ya Debbie Patrocinio kumwokoa kwa kutumia mwanasesere wa nyoka wa Lisa Graciano.
ReplyDeleteNdani ya chumba, akiwa bado amechanganyikiwa, akiwa hajui Debbie alikokwenda, Murphy alisikia walinzi wakipiga kelele nje. Kamanda huwa anakuwa shetani nyakati kama hizo. Alibeba pumzi. Mikononi mwake akiwa na M16, Debbie kichwani, Murphy alishangaza umati wa watu! Risasi zaidi ya thelathini zilifyatuka katika bunduki, mlango wote ukabomoka – ndani ya sekunde kumi!
M16 zilizotumiwa na majeshi ya Marekani dhidi ya majeshi ya Vietinamu mwanzoni hadi mwishoni mwa miaka ya sitini ziliitwa M16A1 (ya kwanza kutoka juu kwenye picha) zilizokuwa na chemba ('magazine') fupi zenye uwezo wa kubeba risasi ishirini kwa kila moja kwa wakati mmoja. Bunduki zilizotumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume zinaitwa M16A2, M16A3 na M16A4 (ya pili, ya tatu, na ya nne kwa mfuatano huo) zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini katika chemba zake za STANAG za NATO kila moja kwa wakati mmoja. Murphy, kule Xochimilco, Mexico City, alitumia bunduki mbili za M16A2 kwa wakati mmoja hivyo kutumia risasi zaidi ya thelathini ndani ya sekunde kumi. Bunduki hizi, zilizoanza kufanyiwa utafiti na Chuo Kikuu cha Hopkins mara tu baada ya Vita ya Korea (1950 – 1953) kwa ufadhili wa Jeshi la Marekani, si nzuri sana kuzilinganisha na AR-15 au AK-47; lakini hakuna bunduki nzuri kuliko nyingine, zote zinafanana.
ReplyDelete