132. Hii ni tiba ya kwikwi: Weka maji katika glasi. Kunywa mafunda sita bila kupumua. Tafuta ushauri wa daktari, tatizo likiendelea.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
- 
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
 - 
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
 

'Diaphragm' ni kiwambo nyumbufu cha tumbo kinachotenganisha uvurungu wa tumbo na uvurungu wa moyo na mapafu, chenye jukumu kubwa na la muhimu sana katika mfumo wa upumuaji. Kiwambo hiki kinaponywea, wakati wa kuvuta hewa kutoka nje, uvurungu wa moyo na mapafu (chumba cha moyo na mapafu) hupanuka, hivyo kuruhusu hewa kuingia katika mapafu.
ReplyDeleteKwikwi ni ugonjwa unaotokana na kunywea kusikokusudiwa kwa kiwambo cha tumbo, kitendo kinachoweza kujirudia mara kadhaa ndani ya dakika moja. Hiki ni kitendohiari (kitendohisia) kinachohusisha neva ya fahamu, inayohusika na matendo yanayotokea bila kukusudia; kama vile kupanuka na kunywea kwa mboni za macho wakati wa mwanga mkali na wakati wa mwanga hafifu, chafya, kwikwi, na kadhalika. Kitendohiari kinapotokea husababisha mnyweo wa ghafla na wa nguvu wa kiwambo cha tumbo – kikifuatiwa na kufungwa kwa vitunga mlio vya sauti ('vocal cords') hivyo kusababisha sauti ya 'hik', ambayo ndiyo kwikwi yenyewe.
Chanzo kikuu cha kwikwi ni kula harakaharaka kupita kiasi, kula au kunywa sana, magonjwa yanayoathiri neva za kiwambo cha tumbo, upasuaji wa tumbo, saratani ya ubongo, mafukizo yenye madhara, na baadhi ya dawa za binadamu.
Mara nyingi kwikwi hupona yenyewe baada ya muda mfupi na mara nyingi si ugonjwa wa hospitali. Tafuta ushauri wa daktari kama kwikwi itaendelea kwa zaidi ya masaa matatu, au kama itakusumbua wakati wa kula au wakati wa kulala.
Zipo tiba mbadala nyingi za kwikwi mbali na dawa za hospitali: kubana pumzi, kunywa maji kwa mkupuo, kuachama na kutoa ulimi nje kwa kadiri utakavyoweza, kula limau, kusukutua maji. Lakini nzuri zaidi ni kunywa makonga sita ya maji bila kupumua, na kuendelea kufanya hivyo mpaka tatizo liishe.
Dawa za hospitali zinazoweza kumsaidia mtu mwenye kwikwi iliyoshindikana ni kama vile 'chlorpromazine hydrochloride' ('Thorazine'), 'haloperidol' ('Haldol'); na 'metoclopramide' ('Reglan') kwa kwikwi sugu, zisizotaka kupona.
Usile kupita kiasi, usinywe kupita kiasi, kama unataka kuzuia kwikwi.