131. Kiswahili ni lugha rasmi ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Ni lugha isiyo rasmi ya nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lugha ya Kiswahili ni mali ya nchi za Afrika ya Mashariki, si mali ya nchi za Afrika Mashariki peke yake. Pia, Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika; pamoja na Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania. Kiswahili ni lugha inayozungumzwa zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine yoyote ile, duniani.
http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...
-
KITENDAWILI CHA KOLONIA SANTITA Shilingi milioni moja za Kitanzania kushindaniwa ndani ya miezi sita kuanzia leo Swali: Kila namba ...
-
Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Jerusalem, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kit...
-
Uwanja wa Ndege wa Copenhagen-Roskilde: uliotumiwa na Tume ya Dunia na Kolonia Santita kwa pamoja – kilometa tisa kutoka katika Kanisa ...

Kiswahili ni lugha ya Kibantu na lugha kuu ya kimataifa ya biashara ya Afrika ya Mashariki ambayo; maneno yake mengi yamepokewa kutoka katika lugha za Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani na Kifaransa, kutoka kwa wakoloni waliyoitawala pwani ya Afrika ya Mashariki katika kipindi cha karne tano zilizopita.
ReplyDeleteLugha ya Kiswahili ilitokana na lugha za Kisabaki za Afrika Mashariki; ambazo nazo zilitokana na Lugha za Kibantu za Pwani ya Kaskazini Mashariki za Tanzania na Kenya, zilizotokana na lugha zaidi ya 500 za Kibantu za Afrika ya Kusini na Kati.
Lugha za Kibantu zilitokana na lugha za Kibantoidi, ambazo ni lugha zenye asili ya Kibantu za kusini mwa eneo la Wabantu, zilizotokana na jamii ya lugha za Kikongo na Kibenue – tawi kubwa kuliko yote ya familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri katika bara la Afrika. Familia ya lugha za Kikongo na Kibenue ilitokana na jamii ya lugha za Kiatlantiki na Kikongo; zilizotokana na familia ya lugha za Kikongo na Kinijeri, ambayo ni familia kubwa ya lugha kuliko zote duniani kwa maana ya lugha za kikabila.
Familia ya lugha ya Kiswahili imekuwepo kwa karne nyingi. Tujifunze kuzipenda na kuzitetea lugha zetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Kikongo-Kinijeri – Kikongo-Kiatlantiki – Kikongo-Kibenue – Kibantu cha Kusini mwa Afrika ya Kusini na Kati – Kibantu – Kibantu cha Pwani ya Kaskazini Mashariki cha Tanzania na Kenya – Kisabaki – Kiswahili.
ReplyDeleteNiger-Congo – Atlantic-Congo – Benue-Congo – Southern Bantoid – Bantu – Northeast Coast Bantu – Sabaki – Swahili.
ReplyDeleteMsingi wa lugha ya Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu, Kireno, Kiingereza, Kihindi, Kijerumani, Kifaransa, na kadhalika.
ReplyDelete