Monday, 23 March 2015

Uchoyo

129. Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo.

http://www.enockmaregesi.wordpress.com 

3 comments:

  1. Mungu alimpa kila mmoja wetu vipawa na vipaji vya pekee kwa ajili ya huduma yake. Kazi yake kwetu hapa duniani ni kutumia vipawa na vipaji vyetu kwa ajili ya huduma ya watu wengine. Kila mmoja wetu ana kitu fulani anachoweza kutoa kwa ajili ya mtu mwingine mwenye shida. Tunaweza kutoa pesa zetu na muda wetu kwa watu maskini. Tunaweza kuwa marafiki kwa watu wapweke au watu wasiojiweza kiafya. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea kwa ajili ya mabadiliko ya watu wengine. Tunaweza kuwa wasuluhishi wa migogoro ya amani. Tunaweza kuwa na upendo usiokuwa na masharti yoyote kwa familia zetu. Tunaweza kufanya kazi za kujitolea au kazi za kuajiriwa kwa uadilifu, uaminifu, heshima, na upendo kwa wengine.

    ReplyDelete
  2. Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa kadiri unavyozidi kujitolea kwa ajili ya watu wengine ndivyo unavyozidi kuwa maskini, lakini hii si kweli. Huduma kwa ajili ya watu wengine huleta maana fulani na ukamilifu katika maisha yetu kwa namna ambayo utajiri, madaraka na mali haviwezi kushindana nao. Mungu hababaishwi na kiasi gani unatoa. Anababaishwa na imani uliyonayo wakati unatoa. Ukitoa kidogo inatosha. Ukitoa kingi inatosha pia.

    ReplyDelete
  3. Kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa. Wengine wana pesa, wengine wana vipaji, wengine wana muda. Vipaji vyote tulivyopewa na Mungu, vikubwa au vidogo, hatuna budi kuvitumia kiukarimu kwa watu wanaovihitaji. Tunapofanya hivyo tunaleta mabadiliko katika dunia kwa ajili ya watu fulani, na tunapata maana halisi ya maisha na toshelezo la moyo katika maisha yetu.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...