Monday, 17 November 2014

KAK

111. Kwa nini tuseme a.k.a na si k.k.k au k.n.k au k.a.k? Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo.

http://www.facebook.com/koloniasantita

2 comments:

  1. A.K.A kirefu chake ni 'Also Known As'. K.K.K kirefu chake ni 'Kadhalika Kikijulikana Kama'. K.N.K kirefu chake ni 'Kadhalika Nikijulikana Kama'. K.A.K kirefu chake ni 'Kadhalika Akijulikana Kama'. Kadhalika, unaweza kusema P.K.K (Pia Kikijulikana Kama), P.N.K (Pia Nikijulikana Kama) au P.A.K (Pia Akijulikana Kama).Tujifunze kuupenda utamaduni wetu, ili vizazi vijavyo visisumbuke.

    ReplyDelete
  2. 'Kolonia Santita' ni kitabu cha Kiswahili. Si Kingereza wala Kihispania. Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo. Kwa nini, kwa mfano, tuseme aka na si kak, pak, kik, pik, kkk, pkk, knk, pnk, ktk, ptk, kvk, pvk, kwk au pwk?
    aka – 'also known as'
    kak – 'kadhalika akijulikana kama'
    pak – 'pia akijulikana kama'
    kik – 'kadhalika ikijulikana kama'
    pik – 'pia ikijulikana kama'
    kkk – 'kadhalika kikijulikana kama'
    pkk – 'pia kikijulikana kama'
    knk – 'kadhalika nikijulikana kama'
    pnk – 'pia nikijulikana kama'
    ktk – 'kadhalika tukijulikana kama'
    ptk – 'pia tukijulikana kama'
    kvk – 'kadhalika vikijulikana kama'
    pvk – 'pia vikijulikana kama'
    kwk – 'kadhalika wakijulikana kama'
    pwk – 'pia wakijulikana kama'.
    http://enockmaregesi.blogspot.com/2013/09/kiswahili.html

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...