Monday, 18 August 2014

Kuomba

98. Kafara ya maombi ni kushukuru wakati wa matatizo. Kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba.

http://www.facebook.com/koloniasantita

7 comments:

  1. Ukipata matatizo kumbuka kwamba Yesu alipata matatizo pia, na kutokana na matatizo hayo mimi na wewe tulipata uhuru. Soma Biblia. Soma nyimbo katika kitabu cha Zaburi zinazomsifu Mungu katika kipindi cha matatizo. Funga na kuomba ukiamini kwamba mapenzi ya Mungu kwetu ni huru, yasiyokuwa na masharti yoyote. Toa msamaha kwa waliokukosea. Ni kitu cha muhimu kujilimbikizia imani katika kipindi cha amani, ili matatizo yakitokea usiweze kuyumba.

    ReplyDelete
  2. Toa msamaha kwa waliokukosea kwa sababu dhambi zilizofanya mkosane zilitoka kwa Shetani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatuna uwezo wa kumshinda Shetani pasipo nguvu ya Roho Mtakatifu.

      Delete
  3. Majaribu na matatizo yana sababu zake – kuwa karibu na Mungu wetu.

    ReplyDelete
  4. Ni vigumu kuishi ka Mungu anavyotaka lkn tukiweza kuishi hivyo tutaishi kwa aman sana hapa duniani, ukimsamee mtu aliyekukosea umesacrifice msamaha wako na Mungu atakubariki.

    ReplyDelete
  5. Kama Yesu, bonge la mfalme, alipata matatizo ili mimi na wewe tupate kukombolewa, wewe ni nani mpaka usiyapate? Yafuatayo ni baadhi ya mafungu katika Biblia yanayozungumzia shukrani kama kafara ya maombi: Zaburi 142:4-7, Isaya 25:4, Luka 23:34, Timotheo 2:8-9, na Waebrania 4:15-16. Madhali tulizaliwa katika dhambi tutajaribiwa. Hatuna uwezo wa kumshinda Shetani pasipo uwezo wa Roho Mtakatifu.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...