Monday, 7 April 2014

Wanaume

79. Wanaume hupenda nyama kwenye mifupa.

http://www.facebook.com/koloniasantita

3 comments:

  1. Morgens hupenda mikono mizuri ya wanawake. Murphy hupenda nyama kwenye mifupa.

    ReplyDelete
  2. Falsafa ya Wanaume inadhihirisha kwamba Murphy hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mtoto wa rais Debbie Patrocinio (ukurasa wa 252 wa 'Kolonia Santita'), kwani Debbie alikuwa mwembamba kuliko mchumba wake Sophia Kaswiga. Murphy alimpenda Debbie kwa sababu ya kazi. Aidha, alimpenda kwa sababu ya matatizo yake. John Murphy hupendelea zaidi wasichana waliojazia kuliko wasichana wembamba, hususan wale wanaojikondesha kwa makusudi.

    ReplyDelete
  3. Hata mwanamke mwembamba ana nyama kwenye mifupa. Falsafa ya Wanaume inalenga wanawake ambao tayari ni wembamba, lakini wanaojikondesha kwa makusudi. Kujikondesha kwa makusudi (kujikondesha kupita kiasi) hupelekea matatizo ya kiafya yanayojulikana kitaalamu kama 'anorexia'. Debbie, baada ya kufiwa na mchumba wake Marciano Moreno Herrera huko Tijuana, mpaka anakutana na Murphy, alikuwa hajala kwa siku saba: hivyo Murphy kufikiria alikuwa na matatizo ya kujikondesha.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...