Monday, 27 May 2013

Kikamilikacho

34. Kikamilikacho si kiimarishwacho.

http//www.facebook.com/koloniasantita

4 comments:

  1. Kitu kikishakamilika hakiwezi tena kuimarishwa, ukilazimisha utakiharibu, you cannot improve on perfection. Rais wa Tume ya Dunia (Boidin Tony Versnick) alitishwa na Umoja wa Mataifa kuondolewa katika wadhifa wake iwapo angeshindwa kumkamata El Tigre ndani ya siku saba bila kujali uaminifu, uthabiti, uvumilivu, uadilifu na uchapakazi wa kazi yake. Mbali na ukamilifu huo katika kazi hata hivyo, kilichokamilika kililazimika kuimarishwa. Versnick alipigana kufa na kupona (ndani ya hizo siku saba) kutetea wadhifa wake, thamani yake ya utu na kutengeneza nafasi nzuri katika historia ya Tume ya Dunia na ya Umoja wa Mataifa na ya dunia kwa jumla – hakuzijali sifa zake za kazi, hakujali sheria, hakujali vitisho vya Umoja wa Mataifa. Lakini pamoja na kazi nzuri aliyofanya, Boidin Versnick alilazimika kujiuzuru wadhifa wake, nafasi yake ikachukuliwa na Makamu wa Rais wa Tume ya Dunia (Jørgen Vestergaard Laursen) aliyekuwa na umri wa miaka sitini na mchapakazi hodari kutoka Denmaki. Versnick alipigana na Kolonia Santita kwa pupa licha ya shinikizo la Umoja wa Mataifa.

    ReplyDelete
  2. kitu kilichokamilika kikiimarishwa na kisiharibike basi ujue kilikuwa hakijakamilika in the first place - nikiwa namaanisha kwamba wakaguzi wa viwango watakuwa hawajakikagua vizuri.

    ReplyDelete
  3. You cannot improve on perfection.

    ReplyDelete
  4. Hiyo ina wafaa watu ambao ni maperfectionist ambao hujitahidi kwa kila hali kuweza kukamilisha mambo.

    ReplyDelete

Roho Yako

289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...