209. Maisha yangu ni kafara ya mafanikio yangu.
Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo lolote na ni tofauti kwa kila mtu. Kama ulivyo uzuri, mafanikio yapo katika macho ya aonaye. Ni jukumu lako kujua mafanikio yana maana gani kwako, na jinsi gani umeyapata mafanikio hayo.
Kufika hapa nilipofika leo nilijitolea vitu vingi na mambo mengi katika maisha yangu. Niliishi katika uhamisho wa kijamii kwa ajili ya mafanikio. Nilijitolea muda. Nilijitolea usingizi. Nilijitolea starehe. Wakati wengine wakienda baa mimi nilikuwa kazini. Wakati wengine wamelala, mimi nilikuwa macho nikifanya kazi. Wakati wengine wakiangalia vipindi pendwa vya televisheni, mimi nilikuwa nikiangalia vipindi visivyopendeka vya televisheni. Wakati wengine wana muda wa kuchezea, mimi nilikuwa nikiyaendesha maisha yangu kwa ratiba maalumu.
Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.
Lakini huwezi kujitoa mhanga bila kwanza kukubaliana na matatizo ya maamuzi yako. Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake.
No comments:
Post a Comment