http://www.facebook.com/koloniasantita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Roho Yako
289. Roho yako inatoka wapi? Ya kwangu inatoka Tanzania. Kwa sababu amani na utulivu ndivyo vitu vya muhimu zaidi katika maisha yangu. ...

-
Mercury Cougar ya John Murphy aliyonunua mwaka 1990 kwa gharama kubwa huko Michigan nchini Marekani. Gari hilo lililorekebishwa kwa ajili ...
-
120. Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu. http://www.enockmaregesi.wordpress.com
-
179. Yesu alipokuwa msalabani watu wengi walimzunguka. Askari wa Kirumi aliyekuwa na chongo, na mkuki, alikuwa na jukumu la kumtesa Yesu ...
Utajiri wa mbinguni ni wa milele na mungu wake ni Yehova. Utajiri wa duniani ni wa muda na mungu wake ni Mammon. Mammon, ambaye hata Yesu alimtaja katika Injili ya Mathayo 6 na katika Injili ya Luka 16, ni mungu wa uchoyo na utajiri wa dunia hii. Mammon kazi yake ni kufanya watu waliokufa kifedha na walio hai kifedha kuwa maskini wa milele ahera. Yesu Kristo alikuwa maskini, ili tuwe matajiri kupitia umaskini wake, lakini kwa sababu alikuwa na imani ya Mungu katika moyo wake alikuwa tajiri. Hivyo unaweza kuwa na utajiri wa mbinguni hapa duniani, ukiikaribisha amani ya Mungu katika moyo wako.
ReplyDeleteImani ina thamani kubwa kuliko mali, wale wenye mali wana thamani machoni pa Mammon, wale wenye imani wana thamani machoni pa Yehova.
ReplyDeleteMammon ni mungu wa pesa wa kuzimu anayesimamia mambo yote ya kifedha ulimwenguni. Ni miongoni mwa mashetani saba waliotupwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kutokea mbinguni akiwemo Ibilisi, Beelzebub, Asmodeus, Leviathan, Amon na Belphegor. Ibilisi ni mungu wa kiburi, Beelzebub ni mungu wa uroho, Asmodeus ni mungu wa zinaa, Leviathan ni mungu wa wivu, Amon ni mungu wa hasira na Belphegor ni mungu wa uvivu. Jukumu la mashetani hawa ni kusimamia kwa uaminifu mkubwa kutokea kuzimu dhambi kubwa saba duniani ambazo ni kiburi, uroho, zinaa, wivu, hasira, uvivu na uchoyo. Dawa ya dhambi hizo ni busara, kiasi, ujasiri, imani, haki, tumaini na upendo.
ReplyDelete